Header Ads

Cr7 anahitaji watoto 7 na ballon d’or 7


Wiki iliyopita Cristiano Ronaldo alimkaribisha mtoto mwingine katika familia yake, huyu alikuwa mtoto wake wa nne kwani tayari alikuwa na Cr7 Junior pamoja na watoto wengine wawili mapacha.
Lakini Cristiano Ronaldo amekiri kwamba idadi hiyo haimtoshi na bado ana mpango wa kuongeza watoto wengine, ataongeza watoto wengine lakini pia ana mpango wa kuongeza tuzo nyingine ya mchezaji bora wa dunia.
Ronaldo amekiri kwamba kwa sasa ana ndoto za kuchukua tuzo ya Ballon d’or kwa mara yake ya 5 huku akisisitiza kwamba hata mwakani pia atafanya kila liwezekanalo ili kuongeza tena Ballon D’Or.
Ronaldo amesisitiza kwamba maisha yake sio tu uwanjani kwani nje ya uwanja kuna vitu bado anavihitaji ikiwemo familia na katika umri wake bado anahitaji kuongeza watu na atahitaji watatu wengine.
Ronaldo hadi sasa ana bao moja tu katika ligi ya La Liga lakini amesema hana wasiwasi wowote kuhusiana na hilo kwani bado ndio kwanza msimu unaanza kupamba moto na amewatoa hofu mashabiki wa Madrid kuhusu uwezo wake.

No comments