C Pwaa ataja wasanii wanne wanaofanya vizuri Bongo kwa sasa
Msanii wa muziki Bongo, C Pwaa amewataja wasanii ambao kwa sasa anaona wanafanya muziki wao vizuri.

Katika mahojiano na kipindi cha Planet Bongo C Pwaa amewataja Country Boy, OMG, Quick Rocka (Switcher Baba) na Chin Bees kama wasanii ambao muziki wao ni mzuri.
Katika hatua nyingine amezingumzia ujio wake mpya kwa kusema kuna kazi zipo tayari ambazo amefanya na Lucci, Mesen Selekta pamoja na P Funk.
“Kuna video ambayo inafanyika sasa hivi tunaangalia tuitoe muda gani kulingana na upepo unavyoenda, unajua siku hizi hutoi wimbo tu lazima uchungulie” amesema C Pwaa.
Post a Comment