Header Ads

BONGO MOVIE NIAJE, WALIMSUSA LULU AU?


Elizabeth Michael ‘Lulu’.
KUNA mambo katika maisha siyo kanuni, lakini utamaduni umeyafanya kuwa kama ndiyo utaratibu. Na haya yako mengi kutegemea na mila za kila jamii. Huwezi kushtakiwa kwa kutokufanya, lakini wanaojumuika na wewe watakesha wakikushangaa.

Jirani yako akipatwa na matatizo, siyo lazima ujitoe na kumsaidia kwa wakati huo, lakini utamaduni wetu unakuona mtu wa ajabu kama ikikutokea hivyo, halafu wewe badala ya kujumuika naye kwa kumfariji, unaalika watu wa ngoma na kufurahi pamoja nao. Hali iko hivyo kwa wafanyakazi wa ofisi moja, wa tasnia moja na hata watu wanaotoka jamii moja.

Kwa mfano, watu wa makabila tofauti kutoka mikoa mbalimbali, wanapokutana katika mkoa au wilaya moja huwa kama ndugu na mmoja wao anapopatwa na matatizo au kuwa na shughuli, wengi hutazamiwa kuwepo.

Katika eneo kama hilo, ingawa huwezi kumpeleka mtu kortini, lakini inapotokea mmoja anashindwa kuhudhuria shughuli hiyo, huonekana kama msaliti kwa wenzake, kitu ambacho kistaarabu kinatia doa. Na kushiriki shughuli ya mtu wa kazini, jamii moja au tasnia moja, haimaanishi kutoa kitu, kwa mfano fedha au kitu chochote, bali ni ile hali ya kuonyesha kuguswa na tukio lililotokea na kibinadamu, kutoa neno la faraja katika mjumuiko huo. Ninasema hivyo baada ya kuguswa na jinsi hali ilivyokwenda kwa msanii mwenye umri mdogo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambaye kwa muda mwingi wa usikilizaji wa kesi yake ya kuua bila kukusudia, alikuwa akienda mahakamani peke yake pasipo sapoti kutoka kwa waigizaji wenzake.

No comments