Andrea Pirlo atundika daluga rasmi
Miaka 38 inaonekana imetosha kwa Andrea Pirlo kucheza soka na sasa kiungo huyo Muitaliano ametundika daluga rasmi na hatocheza tena soka katika timu yoyote ile.
Pirlo ambaye amewahi kuvichezea vilabu vya Inter Milan, Ac Milan na Juventus alianza kucheza soka katika klabu ya Brescia huku pia akiishinda michezo 116 ya timu ya taifa ya Italia.
Andrea Pirlo alishinda kombe la Serie A mara mbili, champions league mara mbili na kikombe cha klabu bingwa dunia akiwa na Ac Milan huku akiwepo katika timu ya taifa Italia iliyobeba kombe la dunia 2006.
Andrea Pirlo pia alikuwa nguzo muhimu wakati Juventus ikishinda kombe la Italia mwaka 2012 hadi 2015 kabla ya kuachana na Juventus nakwenda kucheza ligi kuu ya Marekani MLS mwaka 2015.
Tangu aanze kucheza soka Pirlo amebeba kombe la Italia Serie mara 6, kombe la Copa Italia mara 2, kombe la champions league mara 2 na kbe la dunia mara 1 katika jumla ya michezo 872 aliyocheza.

Post a Comment