Video: Mayanja kuhusu goli la Okwi dakika ya 90 Simba vs Mtibwa Sugar
Kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja amesema, goli la kusawazisha walilopata dhidi ya Mtibwa Sugar limetokana na uwezo binafsi wa Emanuel Okwi na hiyo ni faida ya kuwa na wachezaji wenye uzoefu kikosini.
“Okwi ameweza kutupatia hilo goli kwa individual brilliance (uwezo binafsi), ufundi wake na hapo utaona faida ya kuwa na wachezaji wazoefu, lakini napongeza timu nzima kwa kupambana hadi mwisho”-Jackson Mayanja.
Okwi alifunga goli kwa mkwaju wa adhabu ndogo baada ya Erasto Nyoni kufanyiwa madhambi na mwamuzi kuamuru ipigwe free-kick nje ya box la penati.
Post a Comment