Taarifa rasmi kuhusu majeruhi 4 Simba na mechi watakazokosa VPL
Mchezo wa ligi kuu Tanzania bara Jumapili iliyopita kati ya Simba dhidi ya Mtibwa Sugar ulishuhudia wachezaji wawili wa Simba wakishindwa kuendelea mchezo baada ya kupata majeraha.
Leo Jumanne October 17, 2017, afisa habari wa Simba ametoa taarifa ya maendeleo ya wachezaji wate wanaosumbuliwa na majeruhi na muda watakao kaa nje ya uwanja.
John Bocco
John Bocco aliumia kisigino na kupata maumivu ambayo yatamweka nje kwa siku mbili tatu hali itakayomfanya akose mchezo dhidi ya Njombe Mji Jumamosi October 21, 2017.
Salim Mbonde
Beki wetu wa kati ambaye tunamtegemea sana Salim Mbonde ameumia goti maumivu ambayo yatamfanya akose mechi nne (Njombe Mji, Yanga, lakini pia anaweza akakosa menchi nyingine mbili dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City.)
Ripoti ya madaktari inasema maumivu yake sio makubwa sana lakini anahitaji kukaa nje kwa ajili ya kutumia dawa lakini kama itakuwa vinginevyo basi tutawataarifu.
Said Mohamed ‘Nduda’
Amerejea nchini lakini tofauti na maumivu aliyoyapata Zanzibar ambayo yalipelekea apelekwe India kwa ajili ya upasuaji, alikutwa na tatizo jingine ambalo alikuwa nalo kwa muda mrefu, kwa hiyo madaktari wakamfanyia upasuaji ambapo kwa bahati nzuri wamefanikiwa kwa asilimia 100.
Nduda atakaa nje kwa wiki nane tangu siku aliyofanyiwa upasuaji, maana yake tutaanza kuwa na Nduda kwenye kikosi kuanzia mwezi December.
Shomari Kapombe
Madaktari wameendelea kusisitiza aendelee kupona taratibu matatizo yake ya nyonga inawezekena yalikuwa makubwa tunaamini muda ambao madaktari wamesema akae nje tuendelee kumpa muda na kumvumilia.
Post a Comment