Header Ads

Ronaldo vs Messi: Nani kuwa wa kwanza kutimiza hat tricks 50?


Lionel Messi amethibitisha kwa mara nyingine usiku wa Jumanne kwamba alizaliwa kuucheza huu mchezo unaoitwa soka baada ya kuisadia Argentina kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018.
Magoli matatu ya Messi mwenye umri wa miaka 30 yaliwapa Los Albecelete ushindi wa magoli 1-3 dhidi ya Ecuador na kuipeleka timu yake moja kwa moja nchini Russia.
Hii ilikuwa hat trick ya 44 ya Messi katika soka la ushindani, lakini bado yupo nyuma ya CR7 ambaye ana hat trick 48 katika soka la ushindani – lakini swali ni yupi kAti yao atawahi kutimiza hat trick 50.
Wote wawili walianza siku nyingi kuzifunga hizi hat tricks, huku ya kwanza ya Messi ilikuwa miaka 10 iliyopita katika mchezo wa El Clasico mnamo mwaka 2007, mchezo ambao uliisha kwa sare ya 3-3.
Ronaldo kwa upande wake ilimbidi kusubiri mwaka mmoja baadae, alianza katika mchezo wa ushindi wa Manchester United wa 6-0 vs Newcastle mnamo January 2008.
Hii ndio ilikuwa hat trick pekee ya Ronaldo akiwa na jezi ya Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson – hat tricks nyingine 5 alizifunga akiwa na timu ya taifa ya Ureno na nyingine 42 ameifungia Real Madrid.
Kwenye upande wa timu ya taifa kwa mara nyingine tena, Messi alianza tena kufunga, katika mchezo wa kirafiki wa Argentina dhidi ya Switzerland ambao uliisha kwa 3-1.
Messi ameifungia Argentina hat trick 5 kwa ujumla, wakati nyingine 39 alizofunga akiwa na Barcelona.. 
Hat trick ya kwanza ya Ronaldo katika timu ya taifa ya Ureno ilikuwa katika ardhi ya Uingereza, safari hii huko Northern Ireland wakati Ureno iliposhinda 4-2 katika uwanja wa Windsor Park mnamo mwaka 2013 – mchezo ambao uliipeleka Ureno kombe la dunia 2014.
Msimu huu, Messi tayari ana hat trick 3 na Ronaldo amefunga moja.
Mshambuliaji wa Real Madrid anahitaji hat trick 2 ili kutimiza hat tricks 50, Messi itambidi aendelee kucheza kwenye kiwango cha juu kama atataka kumpiku CR7 na kuwa mchezaji wa kwanza katika kizazi hiki kutimiza hat tricks 50.

No comments