Header Ads

Romelu Lukaku ana rekodi mbovu dhidi ya Liverpool na Jose Mourinho ni kibonde wa Klopp, lakini je Liva hii itaweza izuia United ya sasa?


Tangu mwaka 2014 pale Liverpool walipoipiga Manchester United bao 3 kwa 0 klabu hiyo haijawahi kupata ushindi tena dhidi ya Manchester United kwenye mechi zilizofuata za Premier League.
Jumamosi hii wanakutana tena Anfield na safari hii United wanakuja Anfield wakiwa wanajiamini kwanj katika michezo mitano iliyopita waliyocheza hapo United wameshinda mara 3 wakipata suluhu 1 na kupoteza mara 1.
Kama Liverpool wakipoteza mchezo huu itakuwa habari mbaya kwa Klopp kwani 2014 Brenden Rodgers alifukuzwa baada ya kupata alama 12 katika mechi 8 sawa na ambazo Klopp atazipata kama akipoteza mchezo huu.
Lakini Jurgen Klopp anawapa matumaini Liverpool kutokana na rekodi nzuri mbele ya Mourinho kwani katika michezo 7 Mou amemfunga Klopp mara moja tu huku wakisuluhu mara 3 na Klopp akishinda 3.
Manchester United wanaoonekana kutaka kuendeleza wimbi la ushindi wanaweza kuweka rekodi mpya ya kufikisha alama 22 katika michezo 8 ya Epl kama wakiibuka kidedea dhidi ya Liverpool.
United watakuwa na mshambuliaji wao Romelu Lukaku ambaye siku za usoni anaonekana kujenga urafiki na nyavu na kama akifunga atakuwa mchezaji wa kwanza Epl kufunga mfululizo katika mechi 8 za mwanzo.
Lakini pamoja na ukali wake wote wa kufunga Romelu Lukaku huwa anapata wakati mgumu sana mbele ya Liverpool ambapo katika michezo 7 aliyocheza dhidi ya Liverpool amefanikiwa kufunga bao moja tu.
Manchester United watawakosa Paul Pogba na Maroane Fellaini huku ngome yao ya ulinzi ikiwapa jeuri kubwa ambapo kwa mwaka huu tu 2017 wana clean sheets 17 idadi ambayo hakuna klabu waliyoifikia.
Ni mchezo ambao sio mrahisi kwa pande zote kwani Liverpool pamoja na kumkosa Sadio Mane lakini Mo Salah yupo na Coutinho yupo huku United Ander Herrera anaweza kuanza lakini mashaka makubwa yapo katika eneo la ulinzi la Liverpool linaloonekana kupwaya mno, dakika 90 zitaamua.

No comments