‘POVU’ LAMTOKA HAJI MANARA, AWAITA WAANDISHI AWAWEKEA RUNINGA
Siku mbili baada ya kupitia kwa mchezo wa Yanga na Simba uliomalizika kwenye Uwanja wa Uhuru, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara ameibuka na lingine jipya.
Ofisa huyo ameitisha mkutano na waandishi wa habari na kuelekeza juu ya mchezo huo ikiwa ni siku moja tangu alipomtuhumu beki wa Yanga, Kelvin Yondani kutumia imani za kishirikina kumdhibiti mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi katika mchezo huo.
Manara alitumia ukurasa wake wa Instragrama kutoa tuhuma hizo lakini katika mkutano wake na waandishi wa habari kwenye makao ya klabu hiyo, Msimbazi, leo Jumanne, Manara aliweka runinga na kuonyesha vipande ambavyo timu yake imekuwa ikionewa.
Amesema kuwa kuna maamuzi kadhaa yamekuwa yakifanywa lakini yanaikandamiza Simba ambapo lawama zake nyingi amezipeleka kwa waamuzi akidai wamekuwa hawaitendei haki Simba.
Akizungumza akionekana kuwa na munkari, Manara alisema hajali litakalotokea hasa mitandaoni kwa kuwa anajua atakosolewa lakini anachoamini ni kuwa Simba haijatendewa haki katika badhi ya maamuzi.
“Kuna watu wanalalamika ohh Simba inahitaji mchumi, mchumi wa nini wakati vitu viko wazi hivi, badala mzungumze vitu kama hivi (huku akionyesha kwenye runinga) nyie mnazungumza kuwa angekuwepo Kamusoko.
“Mbona wachambuzi hawachambui mambo kama haya ambayo ni muhimu! Tunanyimwa penati za wazi kabisa lakini mwamuzi hasemi chochote,” alilalama Manara.
Post a Comment