Header Ads

Pique azidi kuchafua hali ya hewa Hispania, bifu lake na Ramos lafika pabaya


Kwa muda mrefu Gerrard Pique amekuwa akiwarushia rushia vijembe Real Madrid, Pique amekuwa akifanya mashambulizi dhidi ya Real Madrid kwa njia ya maandishi na mahojiank hali ambayo humkera captain wa Madrid Sergio Ramos.
Hilo likapita, lakini sasa Pique amekuja na jipya ambalo ni kubwa zaidi. Pique amekuwa mstari wa mbele kuishambulia serikali ya Hispania kwa kitendo chao cha kuzuia kura za maoni za wananchibwa Catalunya kudai uhuru wao.
Pique ambaye ni raia wa Catalunya amesema wazi wazi kutokubaliana na askari wa Hispania jambo ambalo Ramos amelipinga, Ramos anaona sio jambo jema kwa mchezaji wa Hispania kujihusisha sana na masuala hayo.
Ramos anaona anachofanya Pique kinaweza  kuleta mpasuko katika timu ya taifa na kuwagawa Wacatalunya na Wahispania wakati wakiwa timu ya taifa wote wanakuwa kitu kimoja tu.
Wakati hayo yabRamos na Pique yakiendelea tayari mpasuko katika timu ya taifa umeanza kuonekana baada ya hapo jana kuonekana mabango ya kumtukana Gerrad Pique wakati wa mazoezi ya timu ya taifa.
Gazeti moja kubwa nchini Hispania limesema Gerrard Pique ambaye pia ni beki pacha wa Ramos katika timu ya taifa anaweza kulazimishwa kustaafu kuichezea timu ya taifa kutokana na mpasuko huo.
Moja kati ya mabango ambayo yalibebwa wakati wa mazoezi ya Hispania liliandikwa “Pique hatutaki ujitoe timu ya taifa tunataka ufukuzwe” na lingine likiandikwa “mama yangu alisema kama unataka kuwa huru basi ondoka nyumbani”
Timu ya taifa ya Hispania inatarajiwa kuwa na michezo miwili ndani ya siku 3 kuanzia tarehe 6 watakapokipiga na Albania huku siku 3 baadae watakwenda hadi Israel kukipiga na timu ya taifa ya Israel.

No comments