Faustina Charles ‘Nandy’. 
MWANABONGO Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’ amefunguka kuwa hawezi kumchukia msanii Rehema Chalamila ‘Ray C’ kwa sababu ya kutofautiana kwao.

Nandy aliiambia Full Shangwe kuwa, pamoja na Ray C kumtolea povu kuwa asiwe anaimba nyimbo zake, lakini yeye hana kinyongo naye.
Rehema Chalamila ‘Ray C’.
“Sina kinyongo na dada yangu Ray C kwa kile kilichotokea, alichokiposti ni mtazamo wake, sina bifu, sina uhasama naye ,”alisema.