Mwanamke kiongozi wa chama cha soka Sierra Leone akutwa na hatia za rushwa, ampa pesa mumewe na kusafiria
Isha Johansen ndio raisi wa chama cha soka cha Sierra Leone SLFA na mapema mwaka huu alikumbwa na kashfa ya matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo wizi wa pesa alizopata kutoka kwa chama cha soka Afrika CAF.
Baada ya upelelezi sasa mahakama ya nchini humo imemkuta na hatia bibie Isha ambaye pia ni mjumbe katika kamati za chama cha soka barani Afrika CAF na pia FIFA, sasa ana makosa 10 ya kujibu.
Hapo mwanzo upande wa mashtaka ulikuwa ukimtuhumu Johanes kwa makosa sita lakini mbele ya hakimu katika mahakama ya FreeTown makosa ya Johannes yalipanda kutoka 6 hadi kufikia 11.
Lakini pia Johaness anadaiwa kwamba alitumia kiasi cha dolla 3200 kumpa mumewe akidai kwamba alikikopesha chama cha soka cha nchi hiyo kiasi hicho cha pesa jambo ambalo halikuwa kweli.
Post a Comment