Header Ads

MWANA FA AWANANGA WENZAKE


Mwana FA.
MWANA-HIP Hop asiyechuja Hamisi Mwijuma maarufu kama Mwana FA, amewananga wasanii wenzake akidai kuwa wengi wao wanafahamika kwa kiki zao badala ya muziki wao.
Akizungumza na Risasi Vibes, Mwana FA alisema, kwa sasa wasanii wengi nchini kiki zao zina umaarufu kuliko kazi zao, tofauti na enzi zao.
“Kuna baadhi ya wasanii wa sasa hivi, ukiniambia nikutajie kazi zake hata mbili sizijui, lakini ukiniambia nikutajie idadi ya kiki ambazo zimefanywa na wasanii hao ni nyingi mno ninazozifahamu,“ alisema.

No comments