Header Ads

Misri imekuwa timu ya pili Afrika kufuzu Kombe la Dunia 2018, bye bye Uganda


Timu ya taifa ya Misri usiku wa October 8 2017 inaingia katika historia nyingine kwa kuwa timu ya pili kutokea Afrika kufuzu kucheza Kombe la dunia 2018 nchini Urusikwa kuifunga timu ya taifa ya CongoBrazzaville kwa magoli 2-1, ushindi ambao ni pigo ukanda wa Afrika Mashariki tulipokuwa tunaitegemea Uganda.
Magoli ya timu ya taifa ya Misriyakifungwa na Mohamed Salahaliyefunga magoli mawili dakika 64 na dakika za nyongeza 90+5 kwa mkwaju wa penati hiyo ni baada ya dakika ya 87 Congo kusawazisha goli la kwanza kupitia kwa Arnold Bouka Mouttou, hivyo Misri walilazimika kusubiri hadi dakika za nyongeza kukata tiketi.
Ushindi huo sasa unaifanya Misrikuwa timu ya pili Afrika kukata tiketi ya kucheza Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi baada ya Nigeriakufuzu jana, Misri wanafuzu kutokana na kufikisha jumla ya point 12 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote ile katika Kundi E, hiyo inatokana na Uganda jana kutoka sare tasa dhidi ya Ghana mchezo wa Kundi E.
Hadi sasa timu zilizofanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Kombe la dunia 2018 itakayochezwa nchini Urusi ni pamoja na Urusi ambaye ni mwenyeji, BrazilEnglandIranNigeriaJapanMexicoCosta RicaSouth KoreaSaudi ArabiaUjerumaniHispania na Poland.

No comments