Header Ads

Mchezaji wa Simba alinunuliwa viatu na kocha wakati hana pesa


Mchezaji wa zamani wa Simba Uhuru Selemani amemshukuru kocha wake wa zamani aliyemfundisha wakati wapo Msimbazi Milovan Circovic kwa kumuamini tena kwenye kikosi baada ya kusumbuliwa na majeraha kwa muda mrefu.
Kupitia account yake ya Instagram Uhuru amepost ujumbe unaoelezea namna alivyo aminiwa na Milovan licha ya kukaa nje ya uwanja kwa mwaka mmoja akiuza majeraha.
“Heshima kwako Prof. #chico kocha uliye ninyanyua wakati ni chini, niliporejea baada ya kuwa majeruhi kwa mwaka mmoja, hakuna aliyeniamini lakini wewe pekee”-Uhusu Selemani.
Uhuru pia ametoboa kwamba, kuna wakati hakuwa na uwezo hata wa kununua viatu kwa ajili ya kuchezea lakini kocha huyo alimnunulia ili acheze katika kiwango bora.
“Ulininunulia kiatu cha mpira nilipokuwa sina uwezo wa kufanya hivyo. Mungu awe nawe popote ulipo, bado nina kukumbuka na ninakuombea kila wakati Milovan Circovic.”

No comments