Header Ads

MADEE: ILIKUWA NIWE BONDIA


Hamadi Ally ‘Madee’.
RAPA anayetamba na Video ya Semaaliyomshirikisha mwimbaji mahiri Nandy, Hamadi Ally ‘Madee’ ameweka wazi kuwa kabla ya kuibukia katika muziki, ndoto zake zilikuwa ni kupigana ngumi yaani ubondia.
Akipiga stori na Risasi Vibes, Madeealisema ndoto zake za kuwa bondia wa ngumi za kulipwa ziliyeyuka baada ya kubaini kuwa pia alikuwa na kipaji cha muziki.
“Tangu nikiwa mdogo, nilitamani kuwa bondia, nilifanya kazi hiyo huku nikiwa na matarajio makubwa maishani, ndoto zangu ziliyeyuka baada ya kubaini kwamba nina kipaji kikubwa cha muziki, nikaacha na kufanya muziki ingawa naamini siku moja nitarudi kwenye fani hiyo,” alisema Madee.

No comments