Header Ads

Kuelekea Dar derby, vitu ambavyo Simba na Yanga zinafanana baada ya mechi saba VPL


Mjadala mkubwa kwa upande wa soka nchini ni kuhusu October 28, 2017 siku ambayo meci ya watani wa jadi itapigwa watoto wa mjini wanaiita ‘Kariakoo derby’ game ambayo itazikutanisha Yanga na Simba katika mchezo wa VPL mzungunguko wa kwanza
Kabla ya mchezo kuo kupigwa, kuna baadhi ya vitu timu hizi zinafanana kwa kiasi kikubwa sana, idadi ya mechi, pointi, idadi ya mechi za kushinda na sare pamoja na mambo mengine mengi.
Idadi ya mechi
Kila timu imeshacheza mechi saba hadi sasa sawa na timu nyingine za ligi kuu
Pointi
Simba na Yanga zina pointi sawa (15) ambazo kila timu imepata baada ya kucheza mechi saba. Simba ndio inaongoza ligi kutokana na wastani mzuri wa magoli, Simba imefunga jumla ya magoli 19 na huku Aishi Manula akiruhusu magoli manne kwa hiyo wastani wa magoli wa Simba ni 15 wakati Yanga wao wamefunga magoli 10 lakini wamefungwa matatu hivyo kufanya wastani wao wa magoli kuwa saba. Yanga ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi juu ya Mtibwa Sugar ambao pia wana pointi 15.
Mechi za kushinda
Simba
Wameshinda mechi nne kati ya Saba waizocheza, wameshinda michezo mitatu wakiwa uwanja wao wa nyumbani (Uhuru) na mchezo mmoja wakiwa uwanja wa ugenini, Simba wamecheza mechi tatu ugenini huku mechi nne wakizipiga nyumbani.
  • Simba 7-0 Ruvu Shooting
  • Simba 3-0 Mwadui
  • Stand United 1-2 Simba
  • Simba 4-0 Njombe Mji
Yanga
Kama ilivyo kwa Simba Yanga pia wameshinda mechi nne kati ya mechi saba walizocheza, katika mechi nne walizocheza ugenini Yanga wameshinda mechi tatu na kutoka sare mchezo mmoja huku wakishinda mechi moja kati ya tatu walizocheza uwanja wa nyumbani.
  • Njombe Mji 0-1 Yanga
  • Yanga 1-0 Ndanda
  • Kagera Sugar 1-2 Yanga
  • Stand United 0-4 Yanga
Mechi za sare
Simba
Imetoka sare katika mechi tatu, kati ya hizo michezo miwili wakiwa ugenini na mchezo mmoja wakiwa kwenye uwanja wa nyumbani
  • Azam 0-0 Simba
  • Mbao 2-2 Simba
  • Simba 1-1 Mtibwa Sugar
Yanga
Katika mechi tatu walizotoka sare, michezo miwili ni kwenye uwanja wao wa nyumbani huku mechi moja wakibanwa ugenini.
  • Yanga 1-1 Lipuli
  • Majimaji 1-1 Yanga
  • Yanga 0-0 Mtibwa Sugar

No comments