Header Ads

‘Kamati ya ufundi’ ilizuia Simba kuvaa jezi Nyeupe Shinyanga


Baada ya Stand United na Simba kuvaa jezi zinazolalamikiwa kufanana wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa jana Jumapili, October 1, 2017 kwenye uwanja wa Kambarage, ShaffihDauda.co.tz imefanya utafiti kwa nini timu hizo ziliruhusiwa kucheza huku jezi zao zikiwa zinafanana kwa rangi.
Katika kikao kabla ya mchezo (pre match meeting) iliyohudhuriwa na viongozi wa vilabu vyote (Stand United na Simba) pamoja na kamisaa wa mchezo Jovin Bagenda na mwamuzi wa mchezo huo Kinungani Selemani , kwa pamoja waliridhia Simba wavae jezi zenye rangi nyekundu na Stand wavae jezi zao zenye rangi ya machungwa.
Taarifa ambazo Hamisihemedi.co.tz imezipata kutoka vyanzo tofauti ni kwamba, Simba hawakuwa tayari kuvaa jezi zao za ugenini (nyeupe) kutokana na maagizo ya ‘kamati ya ufundi’. Ikabidi kamishna wa mchezo akubali Simba watumie jezi nyekundu kwa sababu jezi za Stand United ni rangi ya machungwa wakiamini zisingewasumbua waamuzi.
Kanuni zinasemaje?
(c) Kila timu inatakiwa kufika na vifaa vifuatavyo:
(i) Sare ya jezi, kaptula na soksi kwa wachezaji wa ndani.
(ii) Sare mbili tofauti za jezi, kaptula na soksi kwa wachezaji wa
ndani, kwa timu mgeni.
(iii) Sare mbili za jezi, kaptula/suruali na soksi za walinda mlango.
(iv) Jezi za mazoezi mchezoni (warming-up).
(v) Kitambaa cha alama ya Nahodha (captain arm band).
(vi) Sare ya Benchi la ufundi (technical bench).
(d) Ni sare zilizoamuliwa kwenye kikao cha maandalizi (pre match meeting)
tu kwa wachezaji na viongozi ndizo zitazoruhusiwa kuvaliwa wakati wa
mchezo.
(e) Kila jezi inatakiwa kuwa na namba kubwa zinazosomeka vizuri zilizo kati
ya namba 1 (moja) hadi 60 (sitini).
(f) Endapo rangi ya sare (jezi) za timu mbili zitafanana, timu ngeni
italazimika kubadili sare yake na endapo moja ya timu sare (jezi) zake
zitafanana na sare za waamuzi, waamuzi watalazimika kubadili. Taratibu
za mabadiliko lazima zijulikane kwenye kikao cha maandalizi (pre match
meeting) tu.
(g) Sare ya mlinda mlango isifanane rangi na sare (jezi) za wachezaji wa
ndanina mlinda mlango wa timu pinzani.
(h) Endapo kutatokea kufanana sare (jezi) za timu wakati wa ukaguzi kabla
ya mchezo kuanza, timu ambayo haikufika kwenye kikao cha kitaalamu
cha maandalizi ya mchezo itawajibika kubadili sare (jezi) zake.
(i) Kamishna atahakikisha timu zinatumia sare kwa mujibu wa rangi za
nyumbani na ugenini kama zilivyoandikishwa na klabu zenyewe kwa TFF.
(j) Timu zitaheshimu uchaguzi wao wa rangi za sare zao kwa michezo ya
nyumbani na ugenini, na endapo itatokea timu ya nyumbani kukosa
uzingativu wa kuwasilisha rangi sahihi kwa sare zake kwa mechi za
nyumbani katika kikao kitangulizi cha mchezo (pre match meeting) timu
ngeni itakuwa na haki ya kwanza ya kuchagua rangi ya sare katika mchezo
husika.

No comments