Header Ads

Ili Lioneil Messi aende kombe la dunia lazima haya yafuatayo yatokee


Kama ni kombe la dunia tu baasi Messi hana bahati nalo, Jumatano asubuhi watakuwa na mchezo wao wa mwisho kutafuta tiketi ya kwenda Urusi lakini wana asilimia ndogo kwenda kombe la dunia na hii itakuwa mara ya kwanza kukosa fainali hizo tangu 1970.
Argentina watasafiri hadi nchini Ecuador huku wakiwa nafasi ya 6 ambapo itawabidi kupigana na kuziombea timu nyingine zipoteze ili waweze kumaliza michuano hiyo katika nafasi tano za juu.
Peru wanacheza na Colombia huku Peru akiwa nafasi ya 5 na alama 25, Colombia wakiwa nafasi ya 4 na alama 26,hii inamaanisha wakipata suluhu katika mchezo wao wa leo huku Argentina wakishinda watawapita na kukaa juu yao.
Ila bado kama Colombia wakawafunga Peru na Argentina akapata hata suluhu watakuwa wamefudhu kombe la dunia, lakini wakipata suluhu kuna Paraguay ambao wanacheza na vibonde Venezuela wanaweza kupita.
Ina maana Colombia akamfunga Peru,Argentina wakasuluhu huku Paraguay wakawafunga Venezuela bado itashuhudiwa Paraguay wakifudhu na Argentina wakabaki, hivyo leo hakuna cha ziada zaidi ya Argentina kuwapiga Ecuador.
Michezo mingine itakayopigwa alasiri ya kesho Brazil watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Chile, huku Uruguay nao watakuwa uwanja wa nyumbani kuikabili Bolivia na huku kinara wa kundi tayari ana uhakika wa kufudhu kwa kombe la dunia.

No comments