Header Ads

Idadi ya majeruhi yazidi kuongezeka Stamford Bridge


Wakati mashabiki wa Chelsea wakiendelea kuuguza kidonda cha kupokea kipigo cha mabao 2 kwa 1 kutoka kwa Crystal Palace klabu ya Chelsea imepokea habari mbaya nyingine baada ya idadinya majeruhi kuongezeka.
Victor Moses ameungana na Alvaro Morata na Ngolo Kante katika orodha ya majeruhi wa Chelsea baada ya Mnigeria huyo kuumia katika mchezo dhidi ya Crystal Palace.
Habari zinasema Moses atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nne ambazo ni sawa na mwezi mmoja hali itakayompelekea kukosa mchezo kati ya Chelsea na Manchester United ambao utapigwa tarehe 5 mwezi ujao.
Kiujumla Moses atakosa michezo saba ikiwemo michezo miwili ya Champions League dhidi ya As Roma na pia Bournemouth, Watford, Everton,Manchester United na West Bromich Albion.
Habari hizi zinaweza kuwa njema kwa mchezaji mpya wa Chelsea Davide Zapaccosta kwani anaonekana anaweza kuwa mtu sahihi kuziba pengo la Victor Moses ambaye msimu huu ulianza vizuri kwake.
Chelsea watakuwa uwanja wa nyumbani wa Stamford Bridge siku ya Jumatano ambapo wataikaribisha As Roma katika muendelezo wa michuano ya Champions League.

No comments