Header Ads

ICELAND NCHI YENYE WAKAZI LAKI TATU NA NUSU ILIYOFUZU KOMBE LA DUNIA


Iceland wamefanikiwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Russia.

Iceland imekuwa ndiyo nchi ndogo zaidi kufuzu Kombe la Dunia.

Wamefanikiwa kufuzu baada ya kuitwanga Kosovo kwa mabao 2-0 baada ya mabao ya Gylfi Sigurdsson na Johann Gudmundsson.


Iceland ina idadi ya wakazi 350,000 tu wakati kabla nchi yenye watu wachache iliyofuzu ilikuwa ni Trinidad & Tobago ambayo ilifuzu mwaka   2006. Idadi ya wakazi wake ni watu milioni 1.3.





No comments