Header Ads

George Weah akaribia uraisi wa Liberia


Matokeo ya uchaguzi nchini Liberia yameanza kutoka huku mshambuliaji wa zamani wa klabu za PSG,Monaco na Chelsea George Weah akionesha kuongoza kwa kura nyingi.
Bado kura nyingi hazijahesabiwa lakini hadi sasa George Weah anaongoza katika majimbo 11 kati ya 15 ambayo tayari kura zao zimekamilika humu idadi kubwa ya majimbo kura zikiwa hazijahesabiwa.
Habari njema na ya matumaini kwa George Weah ni kwamba mpinzani wake mkubwa ambaye pia ni makamu wa raisi wa nchini hiyo Joseph Boakai anaongoza katika jimbo moja tu.
Ili mshindi apatikane inatakiwa apate kura zaidi ya 50% ya kura zote na George Weah inaoenakana wazi anaweza kuwa raisi wa kwanza kuwahi kushinda Ballon D’Or.
Wiki hii kumekuwa na tetesi nyingi kuhusu ushindi wa Weah ambapo hata kocha Arsene Wenger alizipata fununu kuwa Weah ameshashinda uchaguzi na akaamua kumpongeza jambo ambalo halikuwa kweli.

No comments