Header Ads

“Della Madonnina” moja kati ya derby kubwa ulimwenguni kupigwa hii leo


Nchini Italia leo hatumwi mtoto dukani, leo ni siku kubwa kwa Waitalia wemgi kuuona mpambano wenye historia kubwa sana ambapo derby ya Della Madonina ndio habari ya Italia kwa hii leo.
Katika ligi kuu nchini Italia Serie A Inter Millan wanaonekana wababe zaidi wa Ac Millan, michezo 166 waliyokutana vigogo hawa Inter waliibuka kidedea mara 61 huku Ac wakishinda mara 51 na suluhu 54.
Lakini kiujumla timu hizi mbili katika michuano yote zimekutana mara 218 tangu mwaka 1929 na katika mechi hizo Inter Millan wameshinda mara 77 ikiwa ni mara mbili tu zaidi ya Ac Millan walioshinda michezo 75 hali inayoonesha ulinzani kati ya miamba hii.
Katika derby hii kipigo kikubwa kabisa kutokea ilikuwa mwaka 1910 ambapo Inter Millan waliinyuka Ac Millan mabao 5 kwa nunge, japokuwa Ac Millan nao walilipa kipigo hicho mwaka 1960.
Safari hii timu hizi zinakutana katika mazingira tofauti kabisa na mwanzo ambapo safari hii Derby Della Madonnina inawakutanisha Ac Millan na Inter huku zote zinamilikiwa na makampuni ya uwekezaji toka China.
Andriy Shevchenko ndiyo mchezaji anayeongoza kwa kupiga mabao mengi katika Derby hii akifunga mara 14 huku Giussepe Meaza akifuatia na mabao 13 yeye alitafunga mabak haya akizichezea klabu zote mbili.
Juventus na Ac Millan wanafanana sana mambo mengi kwani wote wana makombe 18 ya Serie A, wote wana makombe 15 ya bara la Ulaya lakini pia wote wawili wana makombe 12 ya Copa Italia.
Na kama hufahamu tu ni kwamba katika miaka mitano iliyopita klabu ya Ac Millan imefukuza makocha sita ambapo mapacha wao wa Inter Millan wao wamefukuza makocha watano.
Ac Millan watajaribu kupata ushindi ili kuikaribia Inter walioko nafasi ya pili Serie A huku hawajapoteza mchezo hata mmoja na Ac Millan wako nafasi ya 7 wakiwa na alama 12 huku wakiwa wamepoteza michezo mitatu.

No comments