Header Ads

BAO LA IWOBI LAIZAMISHA ZAMBIA, NIGERIA YAFUZU KOMBE LA DUNIA


Mshambuliaji wa Arsenal, Alex Iwobi amefunga bao pekee lililoiwezesha timu yake ya taifa ya Nigeria kushinda bao 1-0 dhidi ya Zambia.
Ushindi huo umeifanya Nigeria kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwakani nchini Russia.
Nigeria imefikisha point 13 ambazo Zambia pekee wangeweza kulingana na Nigeria kwa point kama wangeshinda leo na kusubiri kuangalia mechi ya mwisho.

Lakini ushindi wa bao hilo la Iwobi dakika ya 73 ambaye alianzia bench, umeihakikishia Nigeria ikitokea Kundi B kucheza Kombe la Dunia mwakani.

No comments