Header Ads

Arjen Robben kaamua kuitosa Uholanzi kuelekeza nguvu zake Bayern


Baada ya kuwafungia Uholanzi mabao mawili hapo jana usiku, winga mkongwe wa timu ya taifa ya Uholanzi Arjen Robben ameamua kustaafu kuitumikia timu ya taifa.
Robben alionekana kukosa raha tangu kabla ya mchezo huo huku kabla ya mchezo akinukuliwa juu ya masikitiko aliyonayo baada ya Uholanzi kuonekana wazi kukosa tiketi ya kombe la dunia.
Baada ya mchezo huo Robben alisema tangu kabla ya mechi hiyo alijua kwamba ulikuwa mchezo wake wa mwisho kuitumikia timu ya taifa na hilo lilimkosesha raha wakati wote wa mchezo.
Arjen Robben anasema walijua kwamba ni ngumu kwao kufudhu kwa kombe la dunia lakini ushindi umewapa kidogo ahueni na kumpa njia nzuri ya kuwaaga Uholanzi.
Arjen Robben ameichezea Uholanzi michezo 96 huku katika michezo hiyo 96 akifunga jumla ya mabao 37 na kutoa jumla ya assist 29 katika michezo yote hiyo.
Robben mwenye miaka 33 amekuwa na timu ya taifa kwa miaka 14 huku kumbukumbu yake ya michuano mikubwa anasema ni mwaka 2010 na 2014 huku akijisifu kwamba pamoja na udogo wa nchi yao lakini wana timu nzuri sana ya taifa.

No comments