Header Ads

Yanga SC kutupa karata yake wikiendi hii VPL


Mikikimikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajia kuendelea kutimua vumbi wikiendi hii wakati mabingwa wa kihistoria wa ‘VPL’, Dar es salaam Young Africans itakapokuwa mwenyeji kuwakaribisha vinara wa ligi timu ya Mtibwa Sugar, ‘Wakata Miwa wa Manungu, Turiani, Morogoro’ katika dimba la uwanja wa Uhuru siku ya Jumamosi ikiwa ni mchezo namba 34 wa duru la tano.
Shabiki kindakindaki wa klabu ya Yanga SC akiwa amebeba bango linalo amasisha watu kuhudhuria Uwanjani 

Siku hiyo ya Septemba 30, vijana wa mholanzi, Hans van Der Pluijm klabu ya Singida United itakuwa mwenyeji Uwanja wa wa Jamhuri Dodoma kuwakaribisha Mabingwa wa kandanda Afrika Mashariki na kati ambao mpaka sasa hawajaruhusu goli lolote, Azam FC
Na huko CCM Kirumba, Mwanza timu machachari, Mbao FC watawakabili Maafande wa Jeshi la Magereza, Tanzania Prisons ‘Wajelajela’.

No comments