WAGONJWA WAZIDI KUHIMIZWA MATIBABU YA BURE
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameendelea kuwasisitizia wakazi wa jiji hilo kuzidi kujitokeza kwa wingi kwenye matibabu yanayotolewa bure katika viwanja vya Mnazi Mmoja kwani siku zilizotolewa zimekwisha na kuongeza kwamba zimebaki siku mbili kabla ya zoezi hilo kumalizika.
Akizungumza na wandishi wa habari, Makonda alisema madaktari kutoka sehemu mbalimbali wameendelea kujitokeza katika viwanja hivyo ili kuongeza nguvu za kutoa matibabu kwa wagonjwa.
Aidha, ameongeza kuwa zoezi la upimaji linaendelea vizuri kwani hakuna mwananchi atakayeweza kufika na asipatiwe huduma.
“Lengo ni kuhakikisha hakuna mwananchi atakaye poteza uhai kutokana na magonjwa yanayoweza kutibika na kuhakikisha wanapata matibabu ya haraka kwa wahitaji wote,” alisema.
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe amewahakikishia wakazi hao ubora wa huduma kwani madaktari wamejizatiti kutumia uwezo wao wote kitaaluma kuhakikisha zoezi linakwenda kama lilivyopangwa.
Post a Comment