Header Ads

WAAFRIKA WATAKAOWIKA NBA 2017/2018


Ekpe Udoh
LIGI ya Kikapu nchini Marekani NBA inatarajiwa kuanza siku chache zijazo huku harakati za usajili zikiwa zimepamba moto. Kila timu kwenye NBA imekuwa na maandalizi yake lakini kuna nyingine zinaonekana kuwa zinaweza kushuka chini kuliko pale zilipomalizia msimu uliopita, huku nyingine zikionekana kujizatiti ili kuwa bora zaidi msimu huu.

NBA Afrika bado inaendelea, lakini chini ni wachezaji kumi bora kutoka Afrika ambao wanatajwa kuwa watawika kwenye NBA msimu huu, wengi wanaaminika watakuwa wakitokea Ukanda wa Mashariki.
Nchini Tunisia kwa sasa huyo ndiye supastaa wao Salah Mejri.
Ekpe Udoh: Staa kutoka nchini Nigeria, Ekpe Udoh, amerejea tena kwenye NBA kwa sasa akiwa na timu ya Utah Jazz, baada ya kudumu hapo mwanzoni na kuondoka kwenda Ulaya.

Hajacheza NBA kwa miaka miwili, lakini kurudi kwake kunaonyesha kuwa anaweza kufanya mambo makubwa sana msimu ujao. Awali aliwahi kuzichezea timu za Golden State Warriors, Milwaukee Bucks, na L.A Clippers, kabla hajaondoka na kwenda nchini Uturuki kwenye timu ya Fenerbahce, amerudi Jazz kuziba pengo la Gordon Hayward na anaaminika kuwa atakuwa mshambuliaji mahiri mwa msimu huu.

Salah Mejri: Nchini Tunisia kwa sasa huyo ndiye supastaa wao Salah Mejri, yupo kwenye mwaka wake wa mwisho na timu ya Dallas baada ya kusaini miaka mitatu.

Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34, hakuwa bora sana kwenye miaka yake miwili iliyopita, akiwa alianza michezo sita tu kwenye msimu wake wa kwanza, lakini msimu wa pili aliwika zaidi baada ya kucheza michezo 73 na kuanza kwenye michezo 11. Anaamini kuwa anaweza kuonyesha umwamba wa hali ya juu msimu huu ili apewe mkataba mpya, lakini kama hatasaini bado Mavericks wameshaonyesha nia ya kumtaka.

Luc Mbah: Mshambuliaji kutoka nchini Cameroon,

Luc Mbah, ni mchezaji mwingine ambaye anapewa nafasi kubwa sana ya kuwika kwenye NBA akiwa na kikosi cha Rockets. Mbah ni kati ya Waafrika ambao wanatajwa kuwa wataonyesha kiwango kizuri kwenye NBA kutokana na kazi aliyofanya msimu uliopita.

Faida kubwa kwake ni kwamba anaweza kucheza nafasi tofautitofauti uwanjani kitu ambacho kinaweza kumpa nafasi kubwa ya kuwa bora na kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa miaka mingine mingi. Tayari mwenyewe ameshasema anataka kuonyesha kiwango cha juu zaidi msimu huu na kuwa na takwimu bora kuliko mingine yote.

Cheick Diallo: Achana na mambo mengine yote, lakini ukweli Diallo anapewa nafasi kubwa ya kuwika kwenye NBA msimu huu. Msimu uliopita haukuwa bora sana kwake baada ya kucheza michezo 17 tu kwenye timu yake ya New Orleans Pelicans, lakini pia hakuanza kwenye mchezo hata mmoja, jambo ambalo linaonyesha kuwa mwaka huu hatakiwi kuuchezea.

Hakuwa na wastani mzuri wa pointi msimu uliopita kwani alimaliza kwa kuwa na wastani wa 5.1 kwa mchezo, wastani ambao ulikuwa hauridhishi. Tayari ameshasema kuwa anataka kuona mwaka huu anakuwa bora kuliko mwaka jana, jambo zuri hapa ni kusubiri.

Emmanuel Mudiay: Huyu ni mchezaji mzaliwa wa Congo DR ambaye bado ana miaka miwili ya kutumika kwenye NBA. Alianza kwa wastani wa kuanza michezo 66 akiwa na wastani wa pointi 12.8 kwa mchezo na kushuka hadi kuanza michezo 41 wastani wa pointi 11.0, jambo ambalo linamfanya aongeze bidii kwa msimu huu kwa kuwa ndiyo pekee uliobaki kwake.

No comments