SNURA APAGAWISHA MINJEMBA KWA CHUMA MATEMBELE
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Snura Mushi, akiongea na mashabiki wake ndani ya Maisha Basement alipozindulia video ya wimbo wake wa Zungusha aliomshirikisha Christian Bella.
Meneja wa Burudani Maisha Basement, Hemed Kavu ‘HK’, akifanya yake.
Wanenguaji wa Tukunyema na Kinyamasina wakifanya yao.
…Wakiendelea kuwadatisha mashabiki.
Snura (aliyesimama kulia) akiwachezesha wacheza shoo wake mwendo wa kuchuma mchicha.
Mashabiki wakiendelea kupata burudani.
MKALI wa Mduara, Snura Mushi ‘Mamaa Majanga’ juzi aliwapagawisha minjemba kwenye uzinduzi wa video ya wimbo wake wa Zungusha ‘Chuma Matembele’ aliomshirikisha Christian Bella ‘Obama’,katika Ukumbi wa Maisha Basement, Kijitonyama jijini Dar.
Uzinduzi wa wimbo huo uliongozwa na burudani kwa majimama wa Kundi la Tukunyema na Kinyamasina kwa kushindana kukata nyonga jukwaani kwa ajili ya kuchuma mchicha na matembele.huku wanaume wengi
wakionekana kudatishwa na mtindo huo. Wasanii wengine walioshiriki katika uzinduzi huo ni Ester Kiama, Aunt Ezekiel na Iyobo, Shilole, Riyama Ally na wengineo.






Post a Comment