Header Ads

SINGIDA UNITED YA BABU HANS YAAMKA, YAWACHAPA MBAO FC

Kikosi cha Singida United kimefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mbao FC licha ya Singida kutokuwa na kocha wao mkuu Hans Van Der Pluijm.

Kwenye kipute hicho cha Ligi Kuu Tanzania Bara kilichopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma mabao ya Singida United yalifungwa na Mudathir Yahya na Michel Katsvairo wakati lile la Mbao liliwekwa wavuni na Habib Kiyombo.

Hans hakukaa kwenye benchi kwa kuwa aatumikia adhabu ya kufungiwa ambayo aliipata msimu uliopita alipokuwa akiinoa Yanga.

Ushindi huo umekuja baada ya kufungwa mabao 2-1 katika mchezo uliopitadhidi ya Mwadui.

No comments