Header Ads

SIMBA WATAMBA WANAIFUATA STAND KWENDA KUCHUKUA POINTI ZAKE TATU



Simba wametamba kuwa wako vizuri na wataondoka Ijumaa kwenda Shinyanga kuivaa Stand United.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema mambo yanakwenda vizuri katika kambi yao ya Mwanza na watakwenda Shinyanga wakiamini pointi tatu ni halali yao.

“Tunaendelea kujiandaa vizuri sana, tunaamini Stand ni timu bora lakini pointi tatu za Stand ni mali yetu.


“Hivyo tunajiandaa kwenda kupambana na kushinda. Pia tuwashukuru sana wanachama na mashabiki wa Simba wa Mwanza ukarimu na kutupokea vizuri,” alisema Manara.

No comments