Header Ads

SIMBA WANAAMINI KAMBI YA MWANZA ITAWASAIDIA POINTI TATU ZA SHINYANGA



 Uongozi wa klabu ya Simba unaamini kambi yao mjini Mwanza, itaisaidia timu yao kubeba pointi tatu dhidi ya Stand United mjini Shinyanga.

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema kambi yao mjini Mwanza, iko katika mpangilio mzuri na wanachotaka ni ushindi wa Shinyanga.

"Baada ya mechi ya Tabora dhidi ya Milambo, tumerejea Mwanza kwa ajili ya kambi na kabla ya mechi tutaenda Shinyanga.

"Tumechagua Mwanza kwa kuwa tunaona ni sehemu ya kambi nzuri na itatusaidia kupata matokeo," alisema.

Simba imecheza mechi ya mwisho ya Ligi Kuu Bara, ilikuwa dhidi ya Mbao FC na matokeo yakawa sare ya 2-2.

Baada ya mechi hiyo Simba ilikwenda kucheza mechi ya kirafiki mjini Tabora na kupata sare ya bila bao.

Sasa timu hiyo imerejea Mwanza kwa ajili ya kambi hiyo ya maandalizi kabla ya kuivaa Stand United wikiendi ijayo.

No comments