Header Ads

Sahau kuhusu kifungo ya Wayne Rooney haya ndio majanga yake mengine


Share this

Ukisema ni mwezi wa tabu kwa Wayne Rooney si vibaya, lakini bado unaweza kuwa mwaka wa tabu maana matukio ni mfululizo.
Baada ya kuonekana hafai Man United na kurejea Everton, Rooney alianza kwa kufunga bao lake la kwanza Tanzania na wengi wakategemea mfululizo wa mabao, mwisho sasa hafungi kabisa.
Wakati hivi karibuni alipata kashfa ya kuwa na mchepuko, jana Rooney kaingia kwenye balaa jingine baada ya kupigwa kiwiko na beki wa Bournemouth, Simon Francis katika mchezo wa jana wa ligi kuu wingereza
Rooney aliumia jicho na kujaa damu, mwisho alibadilishiwa fulana lakini akatolewa ili kumuangalia afya yake.
Mwisho wa mchezo everton ilishinda 2-1 ikiwa nyumbani lakini Rooney akawa hajaisaidia timu yake baada ya kutolewa.

No comments