Header Ads

Matokeo ya mechi za kufudhu kombe la dunia


Uingereza walisafiri hadi taifa la Malta, wakiwa ugenini Waingereza wameibuka kidedea kwa mabao 4 kwa 0 huku Harry Kane akifunga mara mbili, Danny Welbeck akafunga moja huku lingine likifungwa na Ryan Bertand.
Mabingwa wa kombe la dunia timu ya taifa ya Ujerumani nao walikuwa wakiikabili Czech Repuplic katika mchezo ambao Czech walishinda mabao 2 kwa 1 kupitia magoli ya Timo Werner na Mats Hummels huku la Czech likifungwa na Vladmir Darida.
Dernmark wakiwa nyumbani waliifunga Poland mabao 4 kwa nunge huku Thomas Delaney,Christian Eriksenn, Nicolai Jeorgness na Andreass Cornelius wakifunga mabao ya timu ya taifa ya Dernmark.
Nigeria walikuwa wakikipiga na mabingwa wa Afrika timu ya taifa ya  Cameroon na wakashinda bao 4 kwa nunge hukuOdion Ighalo,Mikel Obi,Victor Moses na Kelechi Iheanacho wakifunga mabao ya Nigeria.
Cape Verde waliifunga South Africa 2 kwa 1 kwa mabao ya Nuno Rocha huku lile la South Africa kikiwekwa kimiani na Tokelo Rantie lakini South Africa walilazimika kumaliza pungufu baada ya Erick Mathoho kupewa kadi nyekundu.

No comments