Header Ads

LULU DIVA ALIVYOZICHAPA KAVUKAVU NA NJEMBA


HIT Maker wa ngoma ya Usimwache, Lulu Abasi ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa katika maisha yake, kitu cha kijinga ambacho kamwe hawezi kukisahau maishani ni kitendo cha kuzichapa kavukavu na jamaa mmoja baada ya kupishana kauli.
Akipiga stori na Showbiz Extra, Lulu Diva alisema kuna mambo mengi ambayo ameyafanya maishani mwake, lakini kamwe hawezi kusahau siku hiyo.
“Ilikuwa mara yangu ya kwanza kupigana, kibaya zaidi nilipigana na mtu ambaye nilifahamu fika uelewa wake ni mdogo, kwa kweli ni ujinga ambao huwa naujutia maisha yangu yote, nachukia ugomvi na sikutakiwa kupigana na mtu yule ambaye nisingependa hata kulitaja jina lake,” alisema Lulu Diva.

No comments