Header Ads

Kuna uwezekano huu ndio msimu wa mwisho (2017/18) kumuona Iniesta Barcelona



Mtandao wa express.co.ukumeripoti taarifa ambazo haziwezi kuwa nzuri kwa shabiki wa FC Barcelona kuhusiana na kiungo wao wa kimataifa wa Hispania Andre Iniesta, staa huyo ameripotiwa kuwa mbioni kuihama club hiyo mwisho wa msimu licha ya kupewa ofa mpya.
Iniesta mwenye umri wa miaka 33 mkataba wake na FC Barcelonaunamalizika mwishoni mwa msimu wa 2017/18 lakini ameonesha dalili zote za kutotaka kuongeza licha ya Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu amenukuliwa na Mundo Deportivo kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba na staa huyo.
“Tayari tumeshafikia makubaliano ya mwanzo ya kumuongezea mkataba mpya, natumaini tutakamilisha katika wiki zijazo lakini bado tunaendelea kuzungumza nae kwa sababu ni mchezaji ambaye tungependa kuona akistaafu akiwa hapa atakapojisikia kufanya hivyo” >>>Josep Maria Bartomeu
Josep Maria Bartomeu
Hata hivyo Iniesta amenukuliwa na gazeti la AS baada ya kuulizwa umefikia makubaliano yoyote na Barcelona kuongeza mkataba mpya? jibu lake lilikuwa “Hapana”

No comments