Kuelekea World Cup 2018: Spain wapo tayari kutawala tena soka la dunia
Inaonekana sasa magwiji wa soka barani ulaya wameanza kuonyesha kwamba wana nguvu ya kushindana na wenzao wa Amerika ya kusini kama vile Brazil kwamba wale wanaopewa nafasi kubwa ya kulitwaa taji la dunia, ni wale ambao wamelibeba hivi karibuni.
Ujerumani walionyesha umwamba kwa kushinda mashindano ya kombe la mabara miezi kadhaa nyuma bila kuwa na wachezaji tegemeo wengi,wakiwatumia zaidi makinda – hali inayoonyesha Ujerumani ina utajiri wa vipaji na wataendelea kulitawala soka la ulaya kwa muda mrefu ujao.
Halafu wanakuja France, ambao bahati haikuwa yao kwa kushindwa kutwaa taji la ulaya katika ardhi yao mwaka 2016, walionyesha kiwango kikubwa cha kuridhisha katika mechi za hivi karibubi dhidi ya England na Uholanzi huku wakiwa na kikosi chenye wachezaji wenye vipaji vikubwa wakiwa na umri mdogo – Kylian Mbappe, Ousmane Dembele, Antoine Griezmann, Paul Pogba, N’Golo Kante, Benjamin Mendy, Lemar, na listi inaendelea. Les Bleus na timu nyingine kama Ujerumani wanaonyesha kuwa na utajiri wa vipaji kuelekea mashindano ya dunia.
Lakini Spain wanaonekana kuwa imara zaidi, wikiendi iliyopita waliitendea vibaya Italia kwa kipigo kizito cha 3-0 jijini Madrid — na ingewezekana mchezo ungeisha kwa kipigo cha 6-0 kama nafasi za wazi zote zingetumika — hii inaonyesha muda wa mapito (transition period) umeisha kwa La Roja na sasa wanarudi kuusaka ufalme wa mara ya pili wa Dunia.
Spain walikuwa hawafungiki katika kipindi cha kuanzia mwaka 2008 mpaka 2014, walipotolewa katika hatua ya makundi ya kombe la dunia na kutoa ishara kwamba kwanba enzi zao za utawala zilikuwa zimekwisha, kocha wao Vicente Del Bolsque akaendelea kuifundisha timu hiyo mpaka mwaka 2016, Italy walipowatoa katika round ya pili ya Euro, lakini kocha wa Julen Loptegui amefanikiwa kuirudisha La Roja katika ubora wake na juzo jumamlsi akathibitisha kwa kuinyoosha Italy huku wakicheza soka bora kabisa.
Spain wameanza tena kucheza na system ya kumchezesha “false nine’ – Isco akicheza mbele zaidi huku Alvaro Morata na David Villa wakianzia benchi.
Ukiangalia wachezaji ambao wana ubora wa hali ya juu lakini wamekuwa wanakosa nafasi hata ya kuunda benchi la La Roja, utagundua kikosi cha Lopetegui kina ubora wa aina yake na bado ana options nyingi kwenye benchi na nje ya kikosi. Kwa mara nyingine tena hakukuwa na nafasi ya Cesc Fabregas, Juan Mata na Ander Herrera, moja ya wachezaji bora wa EPL. Gabi – nahodha wa Atletico Madrid mpaka sasa bado anasubiri kucheza mechi yake ya kwanza akiwa na Spain, na huenda mpaka anastaafu asipate nafasi hiyo, ana miaka 34 mpaka sasa — Diego Costa hakupata nafasi safari hii, Fernando Torres na Llorente bado wanawinda nafasi za kurejea kikosini.
Lakini bado kuna makinda kadhaa wanaibuka na kuingia moja kwa moja katika kikosi, kiongozi wao ni Marco Asensio wa Real Madrid. Isco tayari ameshachukua nafasi kikosini, De Gea pia ameshajihakikishia nafasi langoni, lakini pia wakongwe Sergio Ramos na Gerard Pique bado wana nafasi zao kwenye ulinzi – Busquets bado ana nafasi ya kuilinda ngome ya Spain kutokea kwenye safu ya kiungo.
Benchi la Spain ni sababu nyingine ya kujiamini kupata mafanikio wakielekea Russia 2018. Morata alitoka benchi na kwenda kufunga mwishoni mwa mchezo dhidi ya Italy lakini pia kocha Lopetegui anaweza kumtumia kiungo bora wa Atletico Saul Niguez, kiungo wa Bayern Thiago Alcantara na Pedro wa Chelsea
Spain wanajua namna ya kushinda, na wachezaji wengi walioshinda ubingwa wa dunia bado wapo kikosini, hivyo watakuwa na faida ya uzoefu miongoni mwa wachezaji watakaoshiriki World Cup 2018 – ikiwemo Ufaransa ambao nao wana utitiri wa vipaji ila wanakosa uzoefu walionao wacheza wa Hispania.
Ujerumani? Ikiwa watakutana na Spain ni vigumu kutabiri itakuwaje. Mpangilo wa timu, nguvu, kujiamini na ubora wa kikosi cha Joachim Low inawapa nafasi Ujerumani kushindana na Spain japokuwa La Roja ina wachezaji wa zaida ambao wanaweza kubadili mchezo wakati wowote kama Isco, Saul, Asensio.
Mataifa mengine mengine kama Uholanzi na England wao wamekwamba muda wote katika kipindi cha mapito, bado wanasubiri kizazi kipya cha wachezaji wao kurudisha enzi za ushindi – tofauti na Spain ambao wametumia miaka miwili tu kurudi kwenye ubora wao.
Post a Comment