HIVI SNURA HUYO CHURA AKIPUKUTIKA MUZIKI UTAENDELEA
HABARI wadau wa Barua Nzito, niwashukuru nyote kwa maoni na ushauri wenu kila wiki kuhusu safu hii. Mwishoni mwa wiki iliyopita nilibahatika kuhudhuria uzinduzi wa video mpya ya msanii Snura Mushi iliyokwenda kwa jina la Zungusha aliyomshirikisha mkali wa masauti, Christian Bella. Snura ni miongoni mwa wasanii wa kike ambaye ninamkubali, ninampenda kutokana na uwezo wake wa kutunga na kutengeneza nyimbo nzuri ambazo zina uwezo mkubwa sana wa kupenya masikioni mwa mashabiki na kuzipenda.
Kitu kingine nilichojifunza kwa Snura ni muunganiko wake (chemistry) na watayarishaji wake wa muziki akiwemo Abby Dady na wengineo.Tangu wimbo wa Majanga, Chura na nyinginezo wamekuwa wakishirikiana vizuri. Snura, wimbo wako wa Zungusha ni mzuri, unaimbika, unachezeka lakini nilichokigundua kwako unatumia makalio ‘chura’ yako kama silaha ya kila kibao chako. Swali langu kwa dada Snura, hivi siku ‘chura’ wako akipukutika itakuwaje au ndiyo itakuwa mwisho wa wewe kufanya vizuri kwenye gemu? Sina nia mbaya na wewe dada yangu, ila najaribu kukufikirisha kuangalia kwa jicho la tatu zaidi.
Nasema hivyo kwa sababu nimekuwa nikifuatilia kwa karibu sana kazi zako na hata uzinduzi wa wiki iliyopita nilishuhudia mwanzo mwisho kwa jinsi ulivyotumia chura wako kuchuma mchicha na matembele. Achana na wewe, hata wale wanawake ambao walikuwepo kwa ajili ya kushindana kukata mauno kwa ajili ya kunogesha uzinduzi huo, nao walifanya balaa. Ukitaka kuamini kuwa chura siyo silaha kwenye muziki ni pale ambao kundi la wanawake walioshindana kukata nyonga kati ya Kinyamasina na Tukunyema. Baada ya makundi hayo kutifuana jukwaani, kundi lililofanya vizuri na kutuzwa pesa nyingi ni lile la wanawake wenye miili
midogo ila wanazungusha vizuri nyonga zao. Kundi la Kinyamasina ndiyo ninalolizungumzia baada ya kuibuka kuwa washindi kwa kuwabwaga kundi la majimama wenye chura kubwa.
midogo ila wanazungusha vizuri nyonga zao. Kundi la Kinyamasina ndiyo ninalolizungumzia baada ya kuibuka kuwa washindi kwa kuwabwaga kundi la majimama wenye chura kubwa.
Dada Snura, mimi ni miongoni mwa mashabiki wako ambaye nimepata fursa ya kuweza kukuandikia barua yangu kutokana na kile kinachosemwa hata mitaani kwa lengo la kubadilisha ladha ya muziki wako mtamu. Lakini nyuma yangu wako wengi tu wanaotamani kukushauri hivyo lakini hawana fursa hiyo.
Nikiwa bado kwenye uzinduzi niliwasikia pia wadau wengine wakikupongeza kwa wimbo mzuri lakini tatizo lao likawa ni lilelile kama ambalo mimi nimekueleza, kuwa unahitaji ubunifu wa kucheza kwa staili nyingine mbali ya kutingisha tu chura. Mashabiki wanataka mabadiliko zaidi katika uchezaji wako, hata kama chura ndiyo silaha yako, lakini lazima kuwe na kitu cha ziada. Wengi walijaribu kwenda mbali kwa kutolea mfano wa msanii wa muziki wa Nigeria, Yemi Alade, ambaye kila mara anakuwa anabadilika kwenye mtindo wake wa kucheza, hivi karibuni anaonekana akicheza kwa kutumia mguu wake wa kulia kwa kuurudisha nyuma.
Huo ndiyo ubunifu ambao mashabiki wanautaka, siyo kila siku kutumia mijimama inayotingisha chura. Ifike sehemu uwape nafasi na wasanii wengine wenye uwezo wa kukubadilishia ladha ya uchezaji, ninachoamini mitindo ya uchezaji haijawahi kuisha ila kikubwa ni namna gani ya kuumiza kichwa kufanya vizuri zaidi. Sina mtimanyongo na wewe kwa sababu ninakukubali uwezo wako katika burudani ila najaribu kukushauri ili kuboresha vizuri muziki wako na kutowafanya mashabiki wako wakinai kwa ladha i
Post a Comment