Hili ndio bao ambalo Maurcio Pochettino hawezi lisahau
Kila mtu ana nyakati anazozikumbuka sana katika soka, mimi binafsi siwezi kusahau namna ambavyo Manchester City walichukua ubingwa wa Epl mwaka 2012 walipoifunga Qpr mabao 3 kwa 2 pale Etihad.
Lakini kwa kocha Marcio Pochettino naye kama ilivyo kwa mpenda soka yeyote, naye ana kumbukumbu ya mechi na goli ambalo hata iweje hatakuja kulisahau katika maisha yake huku bao hilo likimaanisha kitu kikubwa kwake.
Pochettino yeye kwake ilikuwa mwaka 2014 wakati Tottenham wakikipiga dhidi ya Aston Villa, Poch anaamini mchezo huo uko katika kumbukumbu yak kwani ulikuwa ukiamua hatima yake kubaki Epl ama kuondoka.
Tot walikuwa katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane lakini hadi dakika ya 84 Aston Villa walikuwa wakiongoza, lakini Nacer Chadli aliisawazishia Tottenham kabla ya Harry Kane kufunga bao kwa mkwaju wa free kick dakika ya mwisho ya mchezo.
“Kwangu mimi goli bora linatokana na wakati tuliopo, linafungwa wakati! Kwangu mimi lile goli ndio goli langu ninalolikumbuka zaidi kwani limefanya baadhi kufanya kazi katika timu hii hadi sasa” alisema Pochettino.
Wakati Kane anafunga bao hilo ilikuwa msimu wa kwanza wa Pochettino lakini hadi November timu ilikuwemo katika za kumi la pili katika ligi kuu Uingereza lakini tangu baada ya goli hilo Tottenham waliuwasha moto na kushinda michezo 9 kati ya 14 waliyokuwa wamebakiza.
Katika siku za usoni Tottenham imekuwa klabu inayoleta changamoto kubwa katika ibingwa wa Uingereza, hii leo watakuwa uwanjani Wembley wakiikaribisha Swansea City.
Post a Comment