Header Ads

FT: YANGA 0-0 MTIBWA SUGAR UWANJA WA UHURU


MPIRA UMEKWISHA
KADI DK 90+4 Makapu analambwa kjadi ya njano kwa kumuangusha Mohammed
SUB Dk 90+4 Ismail Aidan anaingia kuchukua nafasi ya Mbonde upande wa Mtibwa
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89 Krosi ya mpira wa adhabu wa Juma Abdul, Mtibwa Sugar wanaokoa vizuri kabisa
Dk 87, Sabato anajaribu kuachia mkwaju mbele ya Dante lakini halikuwa shuti kali
Dk 87, wametolewa nje na kurudi uwanjani baada ya matibabu, mpira unaendelea
Dk 86,Mwashiuya na Makarani wako chini wanatibiwa baada ya kugongana
Dk 83, krosi nzuri hapa ya Yanga, Mtibwa wanaokoa na kuwa kona lakini wanachonga kona dhaifu
SUB Dk 82 Salim Kihingwa anakwenda nje upande wa Mtibwa Sugar na mkongwe Henry Joseph anaingia kwenda kuimarisha ulinzi
Dk 79, MWashiuya anaingia vizuri tena, anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, mpira unamzidi nguvu Tinnoco, unagonga mwamba na Baba Ubaya anaosha, Tinocco yuko chini anatibiwa
SUB Dk 77 Yanga wanamtoa Ngoma aliyeshindwa kuendelea na mchezo, anaingia Juma Mahadhi
Dk 76, mchezo unaendelea kwa Yanga kuchonga kona yao lakini Mtibwa wanaondosha
Dk 75, Ngoma yuko chini anatibwa, kipa wa Mtibwa yuko chini anatibiwa
Dk 73 Kipa Tinnoco wanafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la mwisho la Buswita baada ya shambulizi kali la Yanga katika kipindi cha pili
SUB Dk 71, Daud anakwenda nje kwa upande wa Yanga na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
KADI Dk 69, Gadiel analambwa kadi ya njano kwa kuushika mpira akidhani filimbi ilipigwa
Dk 68, Dante analazimika kumkumbatia Sabato, alistagili kadi lakini mwamuzi hakuona
Dk 66 kona ya Kanoni, Mbonde anagonga kichwa lakini hakuruka, goal kick
Dk 65, shuti kali la Mohammed, kipa Rostand anatema, Sabato anauwahi anapiga tena Yanga wanaokoa na kuwa kona
Dk 64, mpira wa adhabu wa Ajib, unampita beki wa Mtibwa, Ngoma anapiga kichwa unatoka kidogo kabisa pembeni mwa lango la Mtibwa
KADI Dk 63, Mohammed wa Mtibwa analambwa kadi ya njano kwa kumgonga Gadiel kwa mkono
Dk 62 Yanga nao wanapata kona lakini Mtibwa wanaokoa hapa
Dk 61, Mtibwa wanafanya shambulizi jingine, wanapata kona. Inachongwa lakini mpira unamshinda Sabato, goal kick
Dk 59, Yondani anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mbele ya Sabato
SUB Dk 56, Yanga wanamtoa Chirwa ambaye mchezo wa leo umemshinda na nafasi yake inachukuliwa na Kamusoko ambaye anaingiza kuimarisha kiungo
Dk 55, Mtibwa wanagongeana vizuri na kufanya mashambulizi mawili makali likiwemo shuti la Mbonde ambalo Rostand analitema. Sasa Mbonde yuko chini anatibiwa
Dk 51 Buswita anawatoka mabeki wa Mtibwa, anaachia mkwaju mkali hapa kipa anaokoa hapa
Dk 51, Ajib anawachambua vizuri hapa mabeki wa Mtibwa, lakini pasi yake ya mwisho inakuwa mkaa
SUB DK 49 Mtibwa Sugar wanamtoa Hassan Dilunga na kumuingiza Kelvin Sabato Kongwe ambaye ni mshambuliaji
Dk 47, Yanga kupitia Ajibu, Ngoma wanagongeana vizuri lakini Buswita anawekwa chini, faulo. yanga wanapiga Mtibwa wanaokoa
Dk 45, mechi imeanza kwa mwendo wa taratibu kila timu ikionekana inapanga mipango dhidi ya upande mwingine



MAPUMZIKO
DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Juma Abdul analazimika kumuangusha Kihimbwa aliyekuwa anawachambua, Mtibwa inapata mpira wa adhabu lakini hauna madhara kwa Yanga
Dk 42, Dau tena anaachia mkwaju mkali tena lakini anapiga juuuuu
Dk 40, Daud anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, goal kick
Dk 39,Yanga wanapata kona ya tano ya mchezo huu. Inachongwa Tinocco anaokoa na Mbonde anarudi nyuma na kuondosha
Dk 37, krosi safi ya Juma Abdul ndani ya lango la Mtibwa, Kanoni anakaa vizuri na kuokoa hapa
Dk 33, Yanga wanapata kona tena kupitia, inachongwa hapa lakini haina faida
Dk 27, Ajib aanaachia mkwaju mkali wa faulo hapa, Tinocco anafanya kazi ya ziada kuokoa inakuwa kona. Yanga wanachonga lakini Mtibwa wako macho
Dk 25, Chirwa anaingia vizuri hapa lakini mabeki Mtibwa wanamdhibiti na kipa anaokoa. Wachezaji Yanga wanalalamika kuwa Chirwa aliangushwa na mwamuzi anasema twende
Dk 22, Baba Ubaya tena anachonga kona safi tena, anauwahi Mbonde lakini Yanga wanaokoa
Dk 22, Baba Ubaya anachonga kona nyingine safi hapa, Rostand anaokoa kwa juhudi hapa, kona tena
Dk 22, Baba Ubaya anachonga kona hapa, Yanga wanaokoa, kona tena
Dk 21, krozi nzuri ya Mtibwa Sugar, Yondani anafanya kazi ya ziada kuokoa na kuwa kona
Dk 19, Ajib anamtoka mtu na kuingia, anaachia mkwaju wa chinichini, Tinnoco anadaka. Kwa inavyoonekana Ajib yuko vizuri na Mtibwa wasipokuwa makini, atawafunga au kusababisha bao
Dk 17, Yanga wanachonga kona safi kabisa, lakini Baba Ubaya anaondosha hapa
Dk 17, Ajib anaachia mkwaju mkali hapa, kipa Tinocco anafanya kazi ya ziada kuokoa, kona ya kwanza ya mchezo
Dk 14, Chirwa anatoa pasi kwa Ngoma akiwa ndani ya 18 inamkanganya kutokana na spidi ya mpira. Goal kick
Dk 12, Mohammed wa Mtibwa anaachia shuti kali nje ya 18, goal kick
Dk 12, Dilunga anaingia lakini Dante anafanya kazi ya ziada kuokoa
Dk 11, Makarani wa Mtibwa Sugar anaachia shuti lakini si kali. Mtibwa Sugar wanafika mara kadhaa, lakini mashuti yao mengi ni butu
Dk 8, Stamili Mbonde anageuka vizuri kabisa mbele ya Yondani, anaachia mkwaju lakini unaokolewa
Dk 6, Makapu anapoteza mpira na Mohamed anaachia mkwaju mkali langoni mwa Yanga lakini hakulenga lango
Dk 5 sasa, Yanga wanaonekana kuutumia upande wa Gadiel kusukuma mashambulizi lakini Mtibwa Sugar wanacheza katikati zaidi
Dk 2, Gadien anagongeana vizuri na Ajib, lakini ndani ya 18 anaanguka na mwamuzi Abdallah Kambuzi anasema twendweee
Dk 1, Mtibwa Sugar wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Yanga lakini Rostand yuko makini, anaokoa
Dk 1, Mechi imeanza kwa kasi na Chirwa anaanza kwa kucheza madhambi dhidi ya Baba Ubaya

No comments