Header Ads

Dayna Apata Funzo Asimulia Alivyotelekeza Akiwa na Mimba


Dayna Apata Funzo Asimulia  Alivyotelekeza Akiwa na Mimba
Msanii Dayna amesema kwamba kitendo cha kupata mtoto kabla hajatimiza umri wa miaka 18 ni tukio ambalo limempa somo kubwa maishani mwake, kwani mpaka sasa anaogopa kuruka ruka.

 Dayna amesema kwamba pamoja na baba wa mtoto wake kumtelekeza, anapambana kuhakikisha mtoto wake anapata mahitaji yake huku akidai hatorudia kutokuwa makini anapoingia kwenye mahusiano.

"Mimi nilikuwa mdogo sana, unajua sisi wanawake tunafundishwa kupenda, nimejifunza sana, huoni mpaka sasa Rahma ana miaka sijui 10 na kitu lakini hana ndugu yake?, kwa sababu napambana kuhakikisha mtoto wangu anapata mahitaji yote.  Mimi nilijifungua nikiwa mdogo sana hata miaka 18 sikufikisha, nilikuwa na chuki na baba wa mtoto wangu sana lakini nilimuomba Mungu aniondolee roho ya chuki kwa sababu hata nikivimba naye yeye ndiyo baba yake", alisema Dayna.
Dayna ambaye kwa sasa ana kazi mpya ya 'Chovya', amesema iwapo baba mtoto wake atakuja kudai mtoto wake atampa bila kinyongo, kwa kuwa yeye ndiye baba halali wa huyo mtoto na wala hakuna mwingine.

No comments