Header Ads

Coutinho, Diego Costa, Sanchez na hawa wengine watarudi mazoezini wakiwa wamenuna


Dirisha kubwa la usajili kwa mwaka 2018 limefungwa rasmi, vilabu vimenunua na kuuza wachezaji. Lakini kuna orodha ya wachezaji ambao ilionekana wazi wanauzwa na walipendwa wauzwe ila dili zao ziliota mbawa.
Michuano ya kufudhu kwa fainali za kombe la dunia imemalizika kwa wiki hii na wikiendi ijayo inabidi watu warejee katika timu zao,nina uhakika hawa wafuatao hawaamini kama wanarudi kwenye timu zao zile zile za msimu uliopita.
Phellipe Coutinho. Nani asiyejua jinsi Coutinho alitamani kucheza pembeni ya Lioneil Messi na Suarez? Aliomba kuuzwa na Barcelona walikuwa tayari kutoa zaidi ya £80m kumnunua lakini Liverpool inadaiwa walitaka £200m, Coutinho anabaki Anfield jambo ambalo ni wazi hajalifurahia.
Alexis Sanchez. Alirejea hapi kabla katika mazoezi na klabu ya Arsenal baada ya kipigo cha 4 kwa 0 toka kwa Liverpool kukaibuka wimbi kubwa la tetesi kwamba anakwenda Man City, lakini Arsenal wamepambana sana na kufanikiwa kuzuia jambo hilo, Sanchez ameichoka Gunners na ni wazi anaweza ondoka bure msimu ujao.
Diego Costa. Huyu ndio roho itamuuma kabisa kurejea Chelsea, Costa aliweka wazi hatarudi Chelsea lakini jana usiku taarifa zinadai amerudi Uingereza kuongea na Chelsea, jina lake halipo kwenye wachezaji wa Chelsea wa Champions League lakini lipo kwa wanaoshiriki Epl, ndoto zake kwenda Athletico Madrid zimezimwa na sasa anarudi huku hana raha.
Ross Barkley. Kinda huyu mtukutu hakuwepo wakati Everton wanakuja Tanzania, pamoja na majeraha aliyonayo lakini Barkley hayupo vizuri na kocha wake Koeman, zilizagaa tetesi anafanyiwa vipimo vya afya Chelsea lakini hadi sasa Barkley ni mchezaji halali wa Everton.
Virgil Van Djik. Huyu hana bahati kwani karibia timu 4 kubwa Epl zilimhitaji na alionekana wazi tangu dirisha la usajili linaanza kwamba anaweza kuondoka Southampton lakini mwisho wa siku Djik amebaki St Marrys.

No comments