Header Ads

BONGO FLEVA IMEHAMIA YOUTUBE


MUZIKI Bongo upo katika utamu na una ladha ya aina yake kutokana na ushindani uliyopo kwa sasa. Yaani wakati soko la muvi likiendelea kudorora, muziki umezidi kukua na kwa sasa ushindani umehamia kwenye mtandao wa YouTube, wanamuziki wakitunishiana misuli kuwa nani anapata ‘views’ wengi katika mtandao huo.
Kwa sasa haijarishi wimbo wako mtaani unaimbwa ama unasikika kwa kiasi gani. Video umefanyiwa Sauz au Mwananyamala mitaa ya Makoroboi hapa Bongo, watu wapo kwenye namba, YouTube wimbonasomaje na umetazamwa na watu wangapi?
Hilo ndilo la msingi kwa sasa. Ndiyo maana ingawa wimbo wa Aslay uitwao Pusha unafanya vizuri mtaani lakini kwenye mitandao siyo gumzo maana hana namba YouTube, hata kwenye kumi bora za wanamuziki wanaokimbiza Bongo hayumo!
Ndicho kilichomkuta Nay wa Mitego na wimbo wake uitwao Makuzi, hapa chini Uwazi Showbiz inakuletea wakali kumi wanaokimbiza kwa sasa Bongo kwenye mtandao wa YouTube.
Ali Kiba- Seduce Me Huyu ndiye kinara wa YouTube kwa sasa Bongo. Wimbo wake wa Seduce Me mpaka gazeti hili linaingia mitamboni siku ya Jumapili jioni ulikuwa umetazamwa na watu wanaozidi milioni 3. 7 huku wimbo wa msanii mwingine wa Bongo Fleva uitwao Zilipendwa umetazamwa na zaidi ya watu milioni 2.9.
R.O.M.A- Zimbabwe Wimbo wa Zimbabwe wa Roma uliofanywa na Produza Joff Master wa Tongwe Records ndiyo unafuata ukishika namba tatu na umetazamwa na watu wanaozidi milioni 1. 3.
Vee Money- Kisela Vee Money ni mwanamuziki wa kike pekee ambaye anaingia kwenye kumi bora za wanamuziki Bongo wanaokimbiza YouTube. Wimbo wake wa Kisela aliomshirikisha Mr. P kutoka Kundi la P Square unashika namba nne na umetazamwa na watu wanaozidi milioni 1.2.
Jux- Utaniua Wimbo huu hauna muda kwenye mtandao huo wa YouTube. Lakini umeweza kufanya vizuri na kuzizidi nyimbo nyingi ambazo zimetoka kabla yake. Unashika namba tano na umetazamwa na watu wanaozidi laki 7. 5.
Hawa nao wamo! Namba sita inashikwa na Joh Makini ft. Davido wimbo Kata Leta ambao umetazamwa na watu wanaozidi laki 6.4 huku Chege na wimbo wake wa Runtown ukitazamwa na watu wanaozidi laki 4.2.
R.O.M.A narudi tena kwenye listi hii safari hii akiwa na Stamina na project yao ya iitwayo Rostam ambapo wamefanya wimbo uitwo Hivi ama Vile. Wimbo huu umetazamwa pia na watu wanaozidi laki 4.2.
Bill Nass anachukua nafasi ta tisa na Wimbo wa Sina Jambo. Wimbo huu umetazamwa na watu laki 3. 8 huku Fid Q akifunga mkia na wimbo wake uitwao Fresh ambao
umetazamwa na watu laki 2. 5. Data hizi ni kabla ya jana Jumatatu!
MAKALA: BONIPHACE NGUMIJE

No comments