Tangu zuio la mchanga wa dhahabu na shaba liwekwe na Serikali mnamoMachi 3, 2017 na kuathiri takribani 35% ya uzalishaji wa mwaka, Acaciaimekuwa na takribani mchanga wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 265 ndani ya nchi kulingana na bei za sasa
Katika kusaidia kukabili hasara hizi,Acacia imeamua kuchukua hatua kadhaa ikiwemo kupunguza uzalishaji katika mgodi wa Bulyanhulu ili kulinda ajira za wafanyakazi na watoa huduma mgodini ambao ni Watanzania.
Kampuni ya Acacia bado ina matumaini katika majadiliano yanayoendelea kati ya Barrick na serikali ikiamini yatapelekea muafaka juu ya zuio la makinikia na mazingira ya uendeshaji yatakayowezesha tathmini mpya ya hali ya uendeshaji kwa siku zijazo.