Header Ads

VIDEO: Maskini Jini Kabula..Adaiwa Kupatwa Uchizi.....Adai yeye ni Mmarekani na Rihanna ni Dada yake....


Ikiwa ni takriban miezi miwili na siku kadhaa tangu kuzagaa kwa ishu za kuugua ugonjwa wa afya ya akili ukiambatana na kuchanganyikiwa kwa mwigizaji wa sinema za Kibongo, hasa kupitia Tamthiliya ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, hatimaye ameibuka na kunena mambo mazito yenye kuumiza juu ya sakata hilo.
Miongoni mwa mambo anayodai kutendewa, Kabula alisema kuwa, alilazimishwa kupimwa Ugonjwa wa Ukimwi ‘ngoma’ kisha akaanzishiwa dozi ambayo hakuwa anajua kinachoendelea.

MACHOZI KABLA YA SIMULIZI
Muda wote Kabula alikuwa akitiririkwa na machozi yaliyobeba hisia na kila tafsiri ya uchungu huku akitamka maneno mengi makali kwa mfululizo (busara imetumika kutoyaanika).
MKASA WENYE KUUMIZA
“Ninakumbuka siku hiyo nilitoka kanisani, wakati huo nikiishi kwa dada aitwaye Angel. Nilipofi ka nyumbani nilishangaa kukuta watu wengi, nikashtuka kwa kudhani kuna msiba, lakini ghafl a nilikamatwa kwa nguvu na kufungwa kamba.

“Niliuliza kuna nini, lakini hakuna aliyenijibu, zaidi ya baadhi yao kuanza kulia. “Nilikuwa na nguvu sana, maana ndugu zangu wa Marekani akiwemo pacha wangu, Mwanamuziki Rihanna wa Marekani (hapa stori inaanza kuwa mchelemchele) walikuwa wameshatuma makombora kuja kuniokoa mimi malaika niliyezaliwa Tanzania kwa bahati mbaya ili kuja kuikomboa nchi hii.
“Wakanipakiza kwenye lori na kunipeleka Muhimbili (hospitalini). Nilikuwa ninalia sana huku
nikipambana nao kwa nguvu zote, kiukweli nilichoka sana jamani (machozi). “Nimeteswa na kuumizwa sana, eti mimi ninaitwa kichaa, kweli eti (jina la mwandishi), mimi ninaweza kuwa
kichaa kwa unavyonifahamu supastaa mkubwa Bongo? Aah! Hii dunia ni katili sana, lakini Mungu hashindwi na jambo,” ndivyo alivyoanza kusimulia Kabula na kuendelea:


SIMULIZI INAKOLEA SASA
“Wakanipeleka Muhimbili. Lakini kabla ya hapo walishanichoma sindano yenye dawa kali na kunilegeza mwili huku wakinilazimisha kumeza dawa, Mungu anajua (kilio).

“Hapo nikapitiwa na usingizi. Nilipozinduka nilijikuta hospitalini, lakini sasa Wamarekani walikuwa wamekizunguka kitanda changu huku wakirekodi matukio yote (picha limeanza mchelemchele tena). “Basi wakaniuliza kama ninalifahamu eneo hilo, nikawajibu ni Ocean Road (Hospitali ya Saratani), wakaitikia ni kweli japokuwa baadaye nilikuja kujua kwamba ni Muhimbili, yaani walinifanya kama zuzu au mdoli mdogo.”

AFUNGIWA WODI YA VICHAA
Kabula aliendelea kusimulia; “Eti cha ajabu nikafungiwa kwenye wodi ya vichaa. Huko nilikutana na giza la ajabu (kimya, kilio na kigugumizi cha hasira). Kulikuwa na wachawi wakiwa uchi wa mnyama, wakijisaidia karibu kabisa na nilipoweka uso wangu. “Ilikuwa kama nipo kuzimu, lakini hata hivyo, nilijitambua kuwa mimi si Mtanzania ila ni Raia wa Marekani na hata Rihanna ambaye ni pacha wangu nilishamwambia, akasema atakuja kurusha makombora ya ajabu nchi nzima iteketee (mchelemchele tena).  “Nikafungwa kwa minyororo, hebu ona nilivyoumia jamani (akifunua gauni na kuonesha alama za kufungwa eneo la mapajani na makovu sehemu mbalimbali mwilini).

ALIFANYIWA HAYA PIA
“Eti nilipimwa damu na kuambiwa nina Virusi Vya Ukimwi, nikapewa vidonge vya kumeza na mimi sikuwa na jinsi zaidi ya kupokea ili niwafurahishe lakini ukweli sina Ukimwi. Kwa kweli sijawahi kupitia kwenye kipindi kigumu kama hiki, wananionea wivu tu kwa kuwa mimi ni mzuri na mrembo kuliko mama yao yule ambaye walimvisha matambara meusi mbele ya moto mkubwa (mchelemchele tena).


HAJAWAHI KUSINZIA
“Unajua sijawahi kusinzia hata kidogo, walinichoma madawa ambayo yamenikosesha usingizi kwa zaidi ya miezi miwili sasa, yaani usingizi hauji kabisa, si unaona nilivyokondeana jamani, nimechakaa kama chokoraa, sijui hatima yangu, lakini ninamuachia Mungu.”

Kabula aliendelea kusimulia kuwa, baadaye alitolewa wodini na kupelekwa maeneo ya Mbagala jijini Dar, lakini kwa kile alichokiita manyanyaso na masimango alitoroka na kukimbilia kwa rafi ki yake kipenzi ambaye ni msanii wa fi lamu za Kibongo, Esha Buheti ambaye alimkuta akijiandaa kwenda Mbezi-Beach ukweni kwake kwa maandalizi ya kujifungua (ana mimba ya miezi tisa na wiki mbili sasa), ambaye alimshauri aende kwa rafi ki yake mwingine aitwaye Naima maeneo ya Magomeni. Alisema kuwa, huko kwa Naima alikaa siku moja kabla ya kutoroka na kufika Ofisi za Global na kusimulia mkasa mzima.

ETI AMETENGWA
Kabula alisema kuwa, watu wengi wamemtenga na wamekuwa wa kwanza kumsema vibaya na wakati mwingine kumcheka kwa jambo ambalo halijui kwani anajiona mzima wa afya. “Watu wengi ni wanafi ki, sina hata mpango nao na sitaki hata kuwasikia kwa kweli,” alisema Kabula.

APELEKWA KITUO CHA POLISI
Baada ya mahojiano maalum ‘yaliyotafuna’ zaidi ya saa tatu, Kabula alisema kuwa, hana pa kwenda na Global ndiyo msaada wake wa mwisho, ambapo viongozi walimkirimia chochote kwa chakula na nauli ambapo walishauriana kumpeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Oysterbay huku ndugu zake wakitafutwa.


ESHA BUHETI ATINGA POLISI
Baada ya mwandishi wetu kumfikisha Kabula kituoni hapo, aliendelea kuwatafuta ndugu zake na rafiki yake, Naima kasha msanii Esha Buheti ambaye ndiye alifi ka pekee usiku wa manane licha ya kuwa mjamzito wa kujifungua wakati wowote ambapo alishauriana na askari na kukubaliana wamuache hapo hadi kesho yake (Alhamisi) kwa utaratibu mwingine.

NDUGU ANENA YA KUSHANAGAZA
Mwandishi wetu alimtafuta dada wa Kabula ajulikanaye kwa jina la Angel ambaye alisisitiza kuwa, suala la Kabula kulala polisi hadi kesho yake lakini alisema imefi ka hatua wamemshindwa kwani anaumwa kwa kiwango kinachokatisha tamaa. “Kabula anaumwa mno jamani, tunacho hadi kibali cha mahakama ili hata akimdhuru mtu asichukuliwe hatua yoyote.

Kinachoshangaza ni kwamba ana kumbukumbu ya matukio yote na asilimia kubwa ya yale aliyokueleza (baada ya kupewa madai ya Kabula), ni kweli kabisa hapa tulipo tunajiandaa kumpeleka nyumbani Mwanza kwa utaratibu mwingine,” alisema ndugu huyo.



ASUBUHI ALIAMSHA DUDE
Alfajiri ya Alhamsi, mwandishi wetu alikuwepo Kituo cha Polisi cha Oyster bay ambapo alimkuta Kabula akiwatolea ‘mbofumbofu’ askari kwa kuwaporomoshea maneno makali yasiyoandikika, jambo lililowashangaza wengi.

NENO LAKE KWA WATANZANIA
“Watanzania wajue mimi siyo kichaa, lakini huu ni mchezo ninaofanyiwa na watu ambao ni wabaya wangu, nimekonda na kuwa siyo Kabula mnayemjua.

“Naombeni mjue kuwa nina matatizo makubwa sana. Nina mateso kama kufungiwa ndani, nisaidieni jamani, simu yangu imezuiwa, nimetengwa na watu wananikimbia, sijui mwanangu yupo katika hali gani, baba yake (Tuesday Kihangala ‘Chuzi’) hana mawasiliano na mimi. “Nimedhalilishwa sana, ila ninakwenda Marekani kushitaki kwa Obama na Magufuli (mchelemchele unaingia tena), nisaidieni,” alisema Kabula.

KUTOKA GLOBAL TV
Kwa mtazamo ambao gazeti hili limeushuhudia kwa Kabula, kuna kila dalili ya kuwepo kwa tatizo kubwa kwani mazungumzo yake hayana mpangilio sahihi hivyo watu wake wa karibu waungane naye katika kipindi kigumu anachopita kwa kuangalia namna ya kumsaidia.

TAZAMA VIDEO:


No comments