Header Ads

Tetesi za usajili barani Ulaya


Klabu ya Barcelona inamuona Mesut Ozil kama mrithi wa Andre Iniesta na wanaweza kujaribu kumsajili kwa £53m endapo watashindwa kumsajili Phellipe Coutinho kutoka Liverpool.
Kelechi Iheanacho tayari anafanyiwa vipimo vya afya katika timu ya Leicester tayari kwa kujiunga nao, usajili wa Iheanacho umeigharimu Leicester City kiasi cha £25m na atatambulishwa rasmi ndani ya saa 24 zijazo.
Wakati Iheanacho anajiunga na klabu ya Leicester City, kiungo wa Manchester City Fernando naye yuko njiani kuondoka City huku yeye akielekea nchini Uturuki kukipiga katika klabu ya Galatasaray.
Kiungo wa klabu ya Everton Ross Barkley itambidi kukubali kupunguziwa kiasi cha mshahara kama yuko tayari kwenda Tottenham, Tot hawako tayari kumlipa Barkley £120,000 kwa wiki kama anavyotaka.
Pamoja na Carlo Ancelotti kusisitiza Renato Sanchez hauzwi lakini kocha wa Liverpool Jurgen Klopp atajaribu kuishawishi Bayern kuwauzia kinda huyo endapo Coutinho atahamia Barcelona.
Kiungo wa Manchester United Marouane Fellaini ameamua kuangalia kwanza nafasi yake ndani ya klabu hiyo lakini atatoa maamuzi kuhusu anapokwenda itakapofika mwezi January mwakani.

No comments