Header Ads

Shamsa Aford Ampongeza Rais Magufuri kwa Kubana Matumizi






Shamsa Aford Ampongeza Rais  Magufuri kwa Kubana Matumizi
Muigizaji wa Filamu Bongo, Shamsa Ford ameonekana kuvutiwa zaidi na sera ya Rais Dkt. John Magufuli ya kubana matumizi.



Kupitia mtandao wa instagram Shamsa ameeleza kuwa kutokana na utaratibu huo wa Rais Dkt. Magufuli kila kijana kwa sasa anafanya kazi kwani hapo awali wengi wao walipenda vya kupewa.

Tunalalamika maisha ni magumu sana labda kwakuwa hatujazoea hii hali..Ila mm nakupongeza sana raisi wangu kwa kazi unayoifanya. kwanza umetusaidia vijana kuwa wabunifu kila siku.Tulikuwa tumezoea kupewa tu na kazi hatufanyi ila kwa sasa naona kila kijana anafanya kazi kwa bidii na kuheshimu pesa vizuri.Hii itasaidia hata kwa uchumi wa nchi kukua kutokana na kwamba kila kijana anafanya kazi kwa bidii..Mungu akubariki sana Raisi wangu na azidi kukulinda kwa kila mwenye nia mbaya na wewe #UZALENDOKWANZA#

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 ambao ulimuweka madarakani Rais Dkt. Magufuli, Shamsa alikuwa akimpigia debe Edward Lowassa ambaye alikuwa akiungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa.

No comments