Header Ads

Raila Odinga awataka wafuasi wake wagome kwenda kazini




Kiongozi wa Muungano wa Vyama vya Siasa Nchini Kenya (NASA), Raila Odinga amewashauri wafuasi wake kutoingia ofisini kuanzia leo jumatatu ili kuonyesha shinikizo la kutokubaliana na matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika hivi karibuni.

Ameyasema hayo jana wakati akihutubia wafuasi wake jijini Nairobi kwa mara ya kwanza tangu kutangazwa kwa matokeo, ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa mshindi kitu ambacho kilipingwa vikali na Odinga.

Aidha Odinga alisema kuwa siku ya Jumanne, muungano wa vyama hivyo utatoa msimamo wake kuhusu mwelekeo watakaouchukua kulingana na kutokubaliana na matokeo hayo kwa madai kuwa yamechakachuliwa.

Rais Uhuru Kenyatta alitangzwa mashindi kwa kura 8,203,290 huku Raia Odinga akipata kura 6,762,224 kitu ambacho muungano huo wa vyama vya siasa unapinga matokeo hayo kwa kusema yamebadilishwa.

Hata hivyo, Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, ambaye alikuwa mpatanishi mkuu baada ya mzozo wa kisiasa nchini Kenya miaka kumi iliyopita, amemshauri Odinga kutumia hatua za  kisheria kutafuta haki kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais kama anaona kaonewa.

No comments