PROF. LIPUMBA: MAALIM SEIF USINIKIMBIE, NJOO OFISINI TUSAMEHEANE
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na msajili wa Vyama Vya Siasa nchini Profesa Ibrahim Lipumba amemtaka Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad kurudi wafanye mazungumzo na kumaliza tofauti.
Profesa Lipumba amesema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Makao Makuu ya ofisi za Chama Cha Wananchi (CUF) zilizopo Buguruni.
Lipumba amemtaka Katibu Mkuu huyo kurudi wafanye mazungumzo na atambue kuwa yeye ndiye Mwenyekiti wa CUF na ndiye boss wake.
“Maalim analalamika lakini malalamiko yake hayana msingi, yeye ni Katibu Mkuu anapaswa kufuata misingi ya Mwenyekiti, anatambua kuwa Mwenyekiti ni boss kwa mujibu wa Katiba ya CUF, Mwenyekiti nipo yeye aje kufanya kazi hapa. Maalim ni mkongwe wa siasa tunataka kuwa na maelewano, nampigia simu hapokei, nasikia saizi akija Dar es Salaam anakwenda uchochoroni huko Magomeni wakati tuna ofisi hapa nzuri, Katibu Mkuu unauzoefu wa kisiasa tufanye majadiliano ofisi zetu ziko hapa njoo tuzungumze” alisisitiza Lipumba
Aidha Lipumba amesema kama Katibu Mkuu wa CUF hatakuja ofisini kwa ajili ya majadiliano na mazungumzo kwa lengo la kumaliza migogoro yao basi Naibu Katibu Mkuu ataendelea kukaimu nafasi hiyo kwa mujibu wa Katiba yao ya CUF.
“Katibu Mkuu akishindwa kutekeleza majukumu yake Naibu Katibu Mkuu anafanya kazi kwa kufuata maelekezo ya Mwenyekiti ataendelea Kukaimu nafasi hiyo mpaka pale Katibu Mkuu atakapokuwa tayari kuja hapa ataruhusiwa kufanya kazi na ofisi yake ipo hapa, akiwa anakuja ofsini anafuata utaratibu na kufuata maelekezo yangu mimi sina shida ila kama hatakuja basi Naibu Katibu Mkuu ataendelea kufanya kazi” alisema Lipumba
Mbali na hilo Lipumba amesema kuwa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) toka kimempokea Mhe. Edward Lowassa wameacha ajenda ya ufisadi na wameiweka kando ajenda hiyo na kusema sasa hivi wao ndiyo ajenda yao hiyo.
Post a Comment