Oxlade Chamberlain kwenda Liverpool ni usajili wa kisoka zaidi kuliko pesa
Neymar amekwenda PSG kwa rekodi ya dunia ya £220m, Osmane Dembele akaenda Barcelona waweka mzigo wa £160m,Morata Chelsea wakatoa £70m na United nao wakatoa £90 kumnunua Lukaku.
Hilo ndio soka mwanangu, pesa mbele mapenzi baadaye. Wachezaji wote hao hapo juu na wengine wengi wamevutiwa sana na kiasi cha pesa ambacho wameahidiwa japo ukubwa na historia za klabu walizoenda pia ni sababu.
Nchini Uingereza inaonekana vijana wengi wadogo waliokulia Southampton wanapaona Anfield kama sehemu nzuri zaidi kutamani kwenda na ndio maana haikuwa ngumu kwa Ricky Lambert, Adam Lallana, Nathan Clyne na hata Sadio Mane kukubali kujiunga na Liverpool.
Ni utani lakini kama kweli kwani pamoja na wachezaji wanaotokea Southampton kuvutiwa na Liverpool lakini inaaminika Liverpool wanawaona vijana wa Southampton kama watu sahihi na wanaoweza kuibeba Liverpool moyoni na kupambana kwa ajili ya klabu.
Jibu ni rahisi sana kwa mzaliwa huyu wa Portmouth, hakutaka pesa! Ox alitaka akaipiganie klabu ambayo aliamini tangu akiwa kijana mdogo kwamba ndio klabu sahihi kwake, Chamberlain anaipenda Liverpool na hakutaka pesa za Chelsea huku akiwa kachoshwa na mzee Wenger.
Post a Comment